kijana wa leo

kijana.jpg

kama kijana,kuna mambo matano muhimu ya kuyafanya na kuyafuata ili kufikia mafanikio ama kuzifikia ndoto zetu.

 

 

  • Kujitambua;jitambue wewe ni nani katika jamii inayokuzunguka,una nafasi gani kuanzia katika hatua ya kifamilia hadi katika jamii mzima inayokuzunguka,una mchango gani kwa wengine,unafanya nini na kina thamani gani kwa wengine.vilevile kujitambua kama mtu mwenye malengo na ndoto katika maisha.
  • Kujiamini;kijana kitu kikubwa kwenye maisha ni kujiamini,yeyote anayetaka mafanikio lazima kujiamini,ili kufikia ndoto zako ni lazima kukutana na changamoto nyingi hivyo ni vyema kujiamini.
  • Imani,imani ni neno kubwa sana lenye maana kubwa,imani ni ule msukumo wa ndani unaokufanya kutokata tamaa,unaokufanya kuamini juu ya unachokifanya kuwa ipo siku utafanikiwa,kujitengenezea imani juu ya kile unachokifanya itakusaidia kuvuka na kuishinda mitihani mingi ya maisha.
  • Kuzishinda tamaa zenye majuto;tamaa inaweza kuwa ya maana ama yenye majuto mwishoni,vijana wengi wanashindwa kujizuia dhidi ya tamaa,tamaa zimeshika asilimia kubwa ya vijana,tamaa hizi ni kama vile ya mwili,ulevi na mambo yafananayo,ishinde tamaa itakayokurudisha nyuma kimaendeleo.
  • Chagua aina ya marafiki wenye mchango kwako;hii inamaa kuwa rafiki mzuri ni yule anayependa mafanikio yako,ni yule anayekupa mawazo mazuri katika maisha na sio yule anayekufanya ama kuchangia kurudisha nyuma maendeleo kwa kukushawishi kufanya mambo yasiyo ya maendeleo.

Hayo ni baadhi ya mambo makuu ya kuyafuata ili kufikia malengo,kama kijana mpenda maendeleo fuata hayo mambo makuu pia mkaribishe kijana mwingine naye apate faida hii,itaendelea hivi punde..

Asante.

 

 

Advertisements